9 Aprili 2025 - 11:19
Zaidi ya watu 25 waliouawa Shahidi na wengine kujeruhiwa katika shambulio la Marekani katika eneo la Magharibi mwa Yemen

Idadi ya Mashahidi katika shambulio la jana usiku la Marekani katika Mkoa wa Hodeidah Magharibi mwa Yemen imeongezeka na kufikia watu 10, na zaidi ya watu 16 wameripotiwa kujeruhiwa.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) - ABNA-, katika muendelezo wa mashambulizi makali ya Marekani katika maeneo mbalimbali ya Yemen, baadhi ya maeneo ya makazi ya watu wa Magharibi mwa Yemen pia yalilengwa jana usiku.

Kwa mujibu wa ripoti ya kanali ya Televisheni ya Al-Masirah ya Yemen, ndege za kivita za Marekani safari hii zilishambulia maeneo ya makazi ya watu katika majimbo ya Hodeidah na Dhamar, hali iliyosababisha mauaji na kujeruhiwa idadi kadhaa ya raia wa Yemen.

Raia wanne waliuawa shahidi na wengine kadhaa kujeruhiwa katika mashambulizi ya anga kwenye kitongoji cha makazi ya watu katika eneo la Al-Hawk katika Mkoa wa Al-Hodeidah Magharibi mwa Yemen, na uharibifu mkubwa ulisababishwa kwenye nyumba na mali za watu.

Kwa mujibu wa Wizara ya Afya ya Yemen, idadi ya Mashahidi katika shambulio la Marekani kwenye eneo la makazi la Mji wa Muqbil Mkoani Hodeidah imefikia watu 6, na idadi ya waliojeruhiwa imefikia 16, na inakadiriwa kuwa idadi ya majeruhi itaongezeka.

Wizara ya Afya ya Yemeni ilitangaza kuwa watoto watatu na wanawake wawili walikuwa miongoni mwa mashahidi wa mashambulizi ya jinai ya Marekani katika eneo la makazi la Muqbil.

Ikilaani jinai hiyo, Kituo cha Haki za Binadamu cha Ain Al-Insaniyah kimesisitiza kuwa mfululizo wa mashambulizi ya umwagaji damu ya Marekani yanafanywa kila siku dhidi ya ardhi na watu wa Yemen. 

Kituo hicho kilibaini kuwa vitendo vya kikatili vya Amerika vimekuwa uhalifu kamili wa kivita ambao unahitaji uwajibikaji wa haraka mbele ya haki ya kimataifa.

Katika jinai nyingine, muungano unaoongozwa na Marekani ulilenga mtandao wa mawasiliano wa eneo la Shawaba katika mji wa Dhibin mkoani Amran, katika jaribio la wazi la kulemaza uwezo wa Wayemen wa kuwasiliana na kukata maisha ya raia wasio na hatia.

Kwa mujibu wa ripota wa Al-Masirah, adui wa Marekani walifanya mashambulizi matatu na kushambulia kwa mabomu mashamba kadhaa Magharibi mwa Mji wa Dhamar, na kusababisha hasara na uharibifu wa mali.

Ndege za kichokozi za Marekani pia zilifanya mashambulizi kadhaa katika jimbo la Abb la Yemen.

Kwa mujibu wa ripoti ya mwandishi wa Al-Masirah katika jimbo la Abb, ndege za kichokozi za Marekani zililenga mtandao wa mawasiliano wa eneo la Jabal Al-Shamahi katika eneo la Badan Mkoani humo mara tatu.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha